KAMPUNI YA BIN SLUM YAKABIDHI MSAADA WA MATAIRI 12 KWA HUDSON KAMOGA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MBULU MKOANI MANYARA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga  kulia akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa kampuni ya Bin Slum kwa mchango wake katika maendeleo ya wilaya ya Mbulu baada ya kampuni hiyo kupitia kwa meneja Mauzo wake Bw. Salum Aljabiry kumkabidhi moja ya matairi 12 ya magari madogo kutoka kwa  Kampuni ya hiyo jijini Dar es salaam .Kampuni ya Bin Slum imetoa msaada huo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu  ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Mkurugenzi wa Harmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga  kulia akipokea moja ya matairi 12 ya magari madogo kutoka kwa Salim Aljabiry Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bin Slum .Kampuni hiyo imetoa msaada huo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu  ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Baadhi ya matairi yanayouzwa na kampuni ya Bin Slum Chang’ombe/sokota jijini Dar es salaam.