BINSLUM NA COASTAL UNION SASA KAZI TU

Binslum akiwa na wadau wake.

 

MFANYABIASHARA na mdau mkubwa wa soka hapa nchini, Nassor Bin­slum, kwa muda mrefu amekuwa mwanafamilia wa mchezo wa soka akijitolea kwa kila hali katika mchezo huo, lengo lake likiwa ni kuona soka nchini Tan­zania linapiga hatua.

Kampuni yake ya Binslum Tyres Company Lim­ited inayouza vi­faa mbalimbali vya magari kama matairi bora aina za Austone ambayo yanavumilia bara­bara za aina zote zenye vumbi au kokoto pamoja na betri za magari za RB Battery, hivi karibuni amere­jea kwenye kikosi cha Coastal Un­ion ya Tangakitakachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu unaotarajiwa kuanza Sep­temba 16, mwaka huu.

Kurejea kwake kume­kuwa faraja kwa timu hiyo iliyopangwa Kundi B, na sasa matumaini yao ni kuo­na wanacheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19.

Mfanyabiashara huyo siku za nyuma aliamua ku­jiondoa ndani ya klabu hiyo kutokana na kuwa na mi­gogoro mingi, lakini sasa amerejea kwa kazi moja tu, kuisaidia kufanya vizuri na kupanda daraja.

Binslum ambaye kampu­ni yake inaidhamini timu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Bara, kwa sasa hana tofauti zo­zote za kimgongano na viongozi wa Coastal Union kutokana na kumaliza tofauti zao.

Kampuni ya Binslum inakum­bukwa mwanzoni mwa msimu wa 2014/15, iliingia mkataba wa udhamini na klabu tatu zili­zopanda daraja kucheza ligi kuu kwa msimu huo am­bazo ni Ndanda, Mbeya City na Stand United.

Katika udhamini wa timu hizo, ilianza kumwaga mamilioni kwenye Klabu ya Mbeya City kwa kuipa zaidi ya Sh milioni 300 na ku­ingia nayo mkataba wa miaka miwili ambao ulimalizika Juni, mwaka jana. Kutokana na kubaini kwamba udhamini huo unalipa ndani ya timu hiyo, wakaongeza mkataba mwingine wa miaka miwili wenye tha­mani ya Sh milioni 300.

Kwa upande wa Stand United na Ndanda, wali­pewa mkataba wa mwaka mmojammoja, ulipomal­izika, hawakuongezewa.

Kabla ya hapo, huko ny­uma alikuwa mfadhili wa siku nyingi wa Klabu ya Coastal Union, lakini baa­daye akaamua kujiweka pembeni kwa kile kilichoe­lezwa ni migogoro ya mara kwa mara ambayo ilikuja kusababisha timu hiyo kushuka daraja mwis­honi mwa msimu wa 2015/16.

 

Binslum akiwa uwanjani.

“Kutokana na kuwa mdau mkubwa wa soka hapa nchini, nimeona si mbaya kuzidhamini timu mbalimbali kwa len­go la kuzisaidia kufikia malengo yao.

“Niliwahi kuidhamini Coastal Union, lakini timu hiyo sikuid­hamini kwa sababu ya biashara, bali mimi ni shabiki wake na ni­likuwa kiongozi kwenye klabu

hiyo hapo zamani, hivyo lengo langu lilikuwa ni kuinua soka kwenye mkoa wangu wa Tanga na klabu yangu niipendayo,” anasema Binslum ambaye haku­wahi kuwa shabiki wa Simba wala Yanga kama ilivyo kwa mashabiki wengi wa soka hapa nchini.

Kutokuwa kwake shabiki wa timu hizo, hakujawafanya Simba na Yanga kuacha kutumia bidhaa zake kwani klabu hizo mara kwa zimekuwa zikinunua matairi ima­ra ya Doublestar kwa ajili ya ma­basi yao na kuwasaidia kusafiri salama mikoani wanapoenda kucheza mechi zao.

Hivi karibuni baada ya kurejea, Meneja wa Coastal Union, Hilal Said Hilal, ameliambia Champi­oni Jumatatu kuwa, wameamua kukaa chini na Binsulm pamoja na wadau wengine wawili wa soka ambao ni Salim Pemba na Swedi Mkwabi na kuwaomba kuwapa sapoti katika masuala yote ya maandalizi ya timu yao. Wakakubali.

“Ni kweli katika kipindi cha hivi karibuni, Coastal hatukuwa na mahusiano mazuri wenyewe kwa wenyewe hali ambayo ili­sababisha tukashuka daraja kwa aibu.

“Tukaona tulikosea, tuka­jirekebisha na sasa tupo kwenye maandalizi kabambe ya kuhak­ikisha tunafanya vizuri katika Ligi Daraja la Kwanza na matumaini yetu ni kucheza ligi kuu msimu wa 2018/19.

“Kitendo cha Binslum na hao wenzake kukubali kutupa sapoti, ni ishara tosha kwamba kwa sasa Wanatanga tumekuwa kitu kimo­ja, kama ujuavyo ligi tunayoenda kushiriki kama huna fedha za kutosha usitegemee kufanya vi­zuri, lakini hao wenzetu wame­kubali kutusaidia kwa kila kitu, kilichobaki wachezaji kuifanya kazi yao ipasavyo.

“Katika suala zima la usajili, tu­mefanya kwa umakini, tumeweza kuchukua wachezaji kumi wazoe­fu ambao waliwahi kucheza ligi kuu kwa muda mrefu akiwemo Hussein Shariff ‘Casillas’ na Athu­man Idd ‘Chuji’,” anasema Hilal.